UHUSIANO WA SADAKA YAKO NA KUSUDI LA MUNGU:

| Makala

Katika kulijua kusudi la mungu aliloweka ndani yako, kumekuwa na njia kadhaa ambazo zimeendelea kufundishwa na watumishi wengi tu kama ambavyo walivyopewa maelekezo na Roho Mtakatifu, na ni maelekezo ambayo yanasaidia sana.

Kitu pekee ambacho natamani kukiongezea hapa, ambacho Roho Mtakatifu pia amenipatia maelekezo binafsi ili kukusaidia wewe ambaye umekuwa na shauku ya kutamani kulijua kusudi lako na kuliishi.

Maswali muhimu ambayo unapaswa kujiuliza wakati wote:

Maisha unayoyaishi ni yako?

Kusudi lako ni lipi?

Unachokifanya ni kusudi lako?

Kwanini upo duniani?

Wewe ni nani?

Haya ni baadhi tu ya maswali machache kati ya mengi ambayo wengi wetu tumekuwa tunajiuliza sana.

Kwanza kabisa jambo la msingi na la kuzingatia pale unapotaka kabisa kulifahamu kusudi la maisha yako, ni lazima urudi kwa {creator},muumbaji wako, ambaye ni Mungu.Yeye Mungu ndiye anayejua kila kitu kuhusu wewe.

Hivi unafahamu kwamba hata sadaka yako inaweza kukujulisha kusudi lako?

Mara nyingi sana tumekuwa tukipata maelekezo binafsi kuhusu kumtolea Mungu sadaka fulani lakini kwa bahati mbaya sana tumekuwa wakaidi, tumegoma kuisikia na kuitii sauti ya Mungu ili tuvuke, Na hii mara nyingi sana inasababishwa na kutokuwa na uelewa kwa kudhani kwamba unamtajirisha na kumfanikisha mtumishi wa Mungu aliyetumwa kukufundisha hivyo, sijajua tangu uache kumtolea Mungu sadaka kwa uaminifu umefanikiwa na kutajirika kiasi gani kwa kumuibia mungu wako sadaka,

Kila anayetamani kulijua kusudi lake ni lazima kanuni hii aizingatie haswa, ndipo atakapovuka hapo.

Tujifunze kwa Baba yetu wa Imani, IBRAHIMU, Ukisoma kitabu cha mwanzo sura ya 22:1 mpaka wa 18 utaona namna ambavyo Mungu alimtokea na kumjaribu kwenye eneo la sadaka, akimtaka Ibrahim amtoe mwanae wa pekee ambaye ni Isaka, mtoto aliyepatikana uzeeni sana ila Mungu anamtaka kama sadaka.

Mungu alikuwa na lengo la kumjaribu Ibrahim kama kweli atakuwa na utii katika eneo hilo, 

Jambo la kujifunza hapa ni kwamba, kabla Mungu hajakuinua na kukupeleka hatua nyingine, ni lazima kuna mtihani ambao atakuletea sio kwa ajili ya kukukwamisha au kukufelisha, bali kuamini moyo wako kama kweli unampenda Mungu na hata atakapokubariki bado utaendelea kumpenda.

Mwanzo 22:1-18 

Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia. 

Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu. Siku ya tatu Abrahamu akainua macho yake, akapaona mahali pakiwa bado ni mbali. 

Abrahamu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena. Basi Abrahamu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja. Isaka akasema na Abrahamu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. 

Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? Abrahamu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja. Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. 

Abrahamu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe. Ndipo malaika wa BWANA akamwita kutoka mbinguni, akasema, Abrahamu! Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, kwa kuwa hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee. 

Abrahamu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo dume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Abrahamu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. Abrahamu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana. 

Malaika wa BWANA akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

Kumbe zipo ahadi binafsi za Mungu kwa mwanadamu ambaye atakubali kuitii sauti yake na kufuata maelekezo katika eneo la kumtolea yeye sadaka.

Mara ngapi Mungu ametaka kutujaribu kwenye eneo la kumtolea sadaka kama ilivyokuwa kwa Ibrahim lakini tumegoma na kukataa, wengine mnadhani labda ni sauti ya shetani kumbe ni Mungu ndiye anataka akujaribu;

Labda umeshaelekezwa sadaka ya 

Mara ngapi tumeitii sauti hii na kumwambia Mungu kuwa tupo tayari!!!!

Ulipokataa na kupingana na sauti hii ya Mungu ndipo ulipojibakisha hapohapo na maisha yako yakawa kama yalivyo leo, ila sio mpango wa Mungu wewe kuwa masikini au kuendelea kuhangaika na maisha fulani ya mateso, Mungu katika mawazo yake anatuwazia yaliyo mema.

Neno lake linasema kwenye kitabu cha Isaya 1:19-20, “Kama mkikubali na kutii, mtakula mema ya nchi, bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga, maana kinywa cha Bwana kimenena haya”

Mungu akusaidie pale utakapoamua kuchukua hatua ya kumuamini na kuitii sauti yake na kufuata maelekezo yake siku zote za maisha yako.

Pastor Innocent Mashauri

SIRI ZA BIBLIA

Madhabahu ya Mtandaoni

{Maarifa ya ki-Mungu}

+255 758 708 804

 


 SADAKA